Lyrics

Nimeahidi Yesu Lyrics

Nimeahidi Yesu Lyrics

Nimeahidi Yesu – kukutumikia
Wewe u Bwana wangu – u rafiki pia
Sitaogopa vita – wewe ndiwe mweza
Sitaiacha njia – ukiniongoza

Imbeni aleluya, aleluya, imbeni
Shangwe kwa Bwana Yesu, ndiye mweza wetu

Dunia i karibu – Bwana siniache
Na mengi majaribu – yako pande zote
Siku zote adui – ni ndani na nje
Bwana Yesu nivute – karibu na wewe

Nikusikie wewe Bwana – nenda nami Bwana
Kelele za dunia – ndizo nyingi sana
Nena kunihimiza – au kunionya
Nena nikusikie – mwenye kuniponya

Umewapa ahadi – wakufuatao
Kwenda uliko wewe – wawe huko nao
Nami nimeahidi – kukutumikia
Nipe neema Bwana – ya kukwandamia

Hatua zako Bwana – na nizikanyage
Wewe u mwenye nguvu – mimi ni mnyonge
Niongoze nivute – nishike daima
Mwishoni niwasili – mbinguni salama ”

Click Here To Download

Msalaba Ndio Asili Ya Mema Lyrics

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *