Nataka Nimjue Yesu Lyrics
Nataka Nimjue Yesu Lyrics
“Nataka nimjue Yesu
Na nizidi kumfahamu
Nijue pendo lake na
Wokovu wake kamili
Zaidi, zaidi
Nimfahamu Yesu
Nijue pendo lake na
Wokovu wake kamili (Repeat)
Nataka nione Yesu
Na nizidi kusikia
Anenapo kitabuni
Kujidhihirisha kwangu
Nataka nifahamu
Na nizidi kupambanua
Mapenzi yake nifanye
Yale yanayompendeza
Nataka nikae naye
Kwa mazungumzo zaidi
Nizidi kuwaonyesha
Wengine wokovu wake ”