Lyrics

Uko Single Lyrics

Uko Single Lyrics – Zabron Singers

“Ukisikia ni harusi tufurahi
Maana sio rahisi kumpata
Vigezo huwa ni vingi kububali
Mara mfupi mweusi, simtaki
Wengine sitaki mweupe
Mara mi nataka mweusi
Hamjui mungu sitaki
Vigezo kwa vigezo
Sasa nimeshapata wangu kipenzi
Kipenzi cha roho yangu
Ndio huyu hapa leo
Namtambulisha kwenu

UKO SINGLE? hapana nishampata wangu
tunataka tujue… hapana nishampata wangu
YUKO WAPI? Huoni mzuri twaendana
JE, YUKO SINGLE? Hapana keshampata wake
UKO SINGLE? Hapana keshampata wake
Yuko wapi, natujue leo? Ni mimi huoni twaendana

Nishike mkono kipenzi, Kwangu wewe ndo kila kitu
Na leo ndio siku yetu, We mzuri kwangu
Kwa wazazi, ukapita, Moyo wangu ukapitisha
Na pastor amekubali, Tufunge ndoa yetu
Ona twapendeza,Tukitembea pamoja
Tuimbe pamoja, Na tufurahi pamoja
Ona hata watu wote, Wamekusanyika hapa
Kutuweka pamoja , Tuje tuishi pamoja

UKO SINGLE? hapana nishampata wangu
tunataka tujue… hapana nishampata wangu
YUKO WAPI? Huoni mzuri twaendana
JE, YUKO SINGLE? Hapana keshampata wake
UKO SINGLE? Hapana keshampata wake
Yuko wapi, natujue leo? Ni mimi huoni twaendana ”

Zabron Singers – Uko Single?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *